Hili lesemekana huku pande zote kwenye kesi zikitao akuli yao ya
mwisho kabla ya mahakama kutoa hukumu dhidi ya mwanariadha huyo.
Pistorius alipatikana na hatia ya mauji ya mpenzi wake Reeva
Steenkamp bila ya kukusudia mwaka jana.
Jaji Thokozile Masipa anatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya
Pistorius Jumanne.
Anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 lakini jaji anaweza kuamua
kumpa kifungo cha nje au hata kumtoza faini.
Jaji ataanza kusoma hukumu Jumatatu na upande wa mashitaka
unataka Pistorius apewe adhabu kubwa kuambatana na kosa lake.
Lakini mawakili wa
Pistorius wameteta wakisema anapaswa kupewa adhabu ndogo kama vile huduma kwa
jamii.
Wanadai kuwa mwanariadha huyo huenda akateswa akiwa jela, hoja
ambayo imepingwa vikali na mkuu wa magereza.
Pistorius aliangua kilio wakli wake aliposema kuwa pesa zake
zimekwisha baada ya kesi yake kufanya kwa mirzi saba.
"sio tu kwamba hana pesa bali anahisi hana tena
matumaini,'' alisema wakili wa Pistorius.
Hii ni kesi yake ya kwanza. Nini kimtendekea mwanamume huyu?
Nyota yake ilikuwa inaanza kung'ara,'' aliongeza bwana Roux.
Wakili alimuomba jaji kumuonea huruma Pistorius wakati
atakapotoa hukumu.
Mnamo siku ya Ijumaa, kiongozi wa mashitaka alikosoa pendekezo
la Pistorius kuikabidhi familia ya Reeva pesa. Hata hivyo familia ya Reeva
ilikataa pesa hizo ikisema ni pesa za uovu.
Bwana Nel pia alisema ikiwa Pistorius atapewa adhabu ya kiungo
cha nje na kuamrishwa kuihudumia jamii, itakuwa ni hujuma kwai adhabu hiyo
itakuwa ndogo sana kulingana na kosa lake.
BBC SWAHILI
Post a Comment