Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Mtoto wa miaka (05) aliyetambulika kwa jina la Isack Jacob Mkazi wa kijiji cha ilundo amefariki dunia baada ya
kuangukiwa na mti uliokuwa unakatwa na wanafunzi wa shule ya sekondari kiwira
iliyopo wilaya ya rungwe.
Tukio hilo limetokea Octoba 16 mwaka huu majira ya saa
11:00 asubuhi huko katika maeneo ya shule ya sekondari kiwira, kata ya
kiwira, wilayani rungwe, Mkoa wa Mbeya.
Inadaiwa kuwa, marehemu alikuwa
akiokota kuni na watoto wenzake vichakani na ndipo aliangukiwa na mti huo na
kupelekea kifo chake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina
msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi
anatoa wito kwa wazazi na walezi kuweka uangalizi wa kutosha kwa watoto wadogo
ili kuepuka madhara yanayoweza kuepukika.
Aidha, anatoa wito kwa jamii kutowaruhusu
watoto wadogo kwenda maeneo ya vichakani porini bila kuwa na watu wazima kwani
ni hatari.
Mwisho
Post a Comment