(Picha Maktaba) |
N a Mwandishi wetu,Moshi
Mgogoro wa kifamilia kuhusu
mwenye haki ya kuzika mwili wa Rosemary Marandu (38), umeingia siku ya 43 leo,
huku ukiendelea kuhifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Mwili wa marehemu huyo
aliyefariki dunia Septemba 4, mwaka huu umehifadhiwa hospitalini hapo na
unalipiwa Sh9,000 kwa siku, gharama ambayo hadi leo imefika Sh387,000.
Akizungumza jana, baba wa marehemu,
Flavian Marandu, alitoa ruksa ya kuzikwa mwili huo, huku akijiweka kando akidai
hana mamlaka ya kuzika mke wa mtu.
Wiki moja iliyopita, mume
wa marehemu, Sigfrid Mlingi alimtuhumu baba mkwe wake huyo kuzuia mwili huo na
baadaye kumtolea lugha chafu.
“Mimi ndiye nilimuuguza
Hospitali ya Mawenzi hadi kunifia mikononi, nilipokwenda Keryo na kuonana na
baba mkwe, akanifukuza,” alidai Mlingi.
Mlingi alisema awali
walikubaliana kumzika Septemba 9 katika Makaburi ya Karanga, Manispaa ya Moshi
lakini baadaye mkwewe alikataa.
Lakini jana, Marandu
alisema: “Huyo ni mke wa mtu...kama kuna mtu ana shida akachukue kibali
akazike, mimi sina kibali,” alisema.
Marandu alisema tangu msiba
huo utokee, ametuma marafiki zake kuzungumza na ndugu ili mazishi hayo
yafanyike baada ya kuridhiwa na mume na mama mzazi lakini hawatoi ushirikiano.
Lakini ndugu mwingine wa
marehemu, Bertha Akwilin alipoulizwa jana, alikiri kuzungumza na Marandu juzi
na kumwelekeza kwenda kuchukua kibali kutoka kwa mtu aitwaye Tesha.
“Ni kweli nimepata bahati
ya kuzungumza na baba (Marandu) na akatoa ruksa hiyo lakini mama wa marehemu na
wana ndugu bado wanatafakari ukweli wa kauli ya Marandu,” alisema.
Post a Comment