Mwenyekiti wa Bajaji jijini Mbeya Ndugu Petro Masasi akizungumza na maderva katika mkutano huo |
Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akizungumza katika Mkutano wa Madereva wa Bajaji jijini Mbeya katika Ukumbi wa Kiwila Motel jijini hapa |
Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Mbeya Ndugu Denis Daud |
Tuko makini kusikiliza |
Mwenyekiti wa Bajaji aliyemaliza muda wake Bw. Ostaazi |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Chama cha Madereva wa Bajaji jijiji Mbeya kimefanya mkutano wa pamoja na Viongozi wa Usalama barabarani Mkoani Mbeya lengo ikiwa ni kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika suala la utoaji wa huduma ya usafiri jijini hapa.
Mkutano huo pia ulihusisha baadhi ya wamiliki wa bajaji pamoja na madereva ambapo mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa kiwila Motel jijini hapa.
Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Usalama Barabarani Mbeya Bi.Butusyo Mwambelo amesema umefika wakati sasa Jeshi la Polisi Usalama Barabarani kuanza kusimamia sheria za usalama barabarani ipasavyo kwani kwa kiwango kikubwa madereva wengi hususani madereva wa bajaji wamekuwa wakivunja sheria na taratibu za usalama barabarani makusudi huku wakifahamu kuwa ni kinyume cha sheria.
Amesema kwa muda mrefu madareva wa bajaji jijini Mbeya walikuwa mfano katika suala la utoaji wa huduma lakini kwa sasa wao ndio wamekuwa kikwazo kikubwa huku wakipitwa na maderava bodaboda ambao ndio walikuwa kikwazo katika suala la utoaji wa huduma ya usafiri.
Amesema idadi kubwa ya madereva wa bajaji wamekuwa wakitoa huduma za usafiri huo pasipo kuwa na leseni pamoja na kubeba abiria kwa mfumo wa mishikaki hali ambayo ni hatari na imekuwa ikichangia kwa kiwango kikubwa kusababisha ajali za barabarani.
Amesema makosa mengine ambayo madereva hao wamekuwa wakiyafanya ni pamoja na kuanzisha vituo bubu vya kupakilia abiria ambavyo havija sajiliwa kisheria .
Amesema hatokubali kuona jeshi la polisi linaendelea kupakwa matope na watu wachache ambao hawataki kufuata sheria za usalama barabarani kwa makusudi .
Hata hivyo Mkuu huyo wa usalama barabarani ametoa agizo kwa madereva hao wa bajaji kuacha mara moja kutumia barabara kuu Meine Road badala yake watumie njia za pembezoni mwa barabara (Service Road) kuanzia sasa pamoja na kusitisha suala la upigaji debe mara wafikapo katika vituo vya daladala.
Kwa upande wake Afisa Mfawidhi wa Sumatra mkoani hapa Ndugu Denis Daud amewataka madereva hao kutoa ushirikiano katika ofisi yake ili kupunguza suala zima la ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababishwa na uzembe wa madereva.
Aidha Mwenyekiti wa Bajaji jijini Mbeya Ndugu Petro Masasi amelishukuru jeshi hilo la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa hatua yao ya kukubali kuonana na madereva hao na kutoa elimu hiyo .
Amesema kutokna na kuwepo kwa changamoto hizo atahakikisha anaitisha mikutano ya mara kwa mara na kukusisha viongozi hao ili kuhakikisha wanatoa huduma stahiki za usafiri kwa wananchi
mwisho
Post a Comment