Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Jamal Malinzi |
Na Boniface Wambura
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatumia salamu za rambirambi vyama vya mpira
wa miguu vya Zambia (FAZ) na Afrika Kusini (SAFA) kutokana na vifo vya Rais
Michael Sata na kipa wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Senzo Meyiwa.
Ametuma
salamu hizo kwa Rais wa FAZ, Kalusha Bwalya na Rais wa SAFA, Danny Jordan na
kuongeza kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya ghafla vya Rais Sata
na kipa huyo wa Bafana Bafana vilivyotokea wiki hii.
Rais
Malinzi amesema kuwa misiba hiyo si pigo kwa Zambia na Afrika Kusini pekee bali
Afrika kwa ujumla kwa vile walikuwa na mchango mkubwa kwa ustawi wa mchezo wa
mpira wa miguu.
Amewaomba Rais Jordan na Rais Bwalya
kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Sata, na familia ya Meyiwa, na
kuzitaka kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha
misiba hiyo mizito kwao.
Rais
Sata (77) alifariki dunia juzi kwenye Hospitali ya King Edward VII nchini
Uingereza alipkuwa kwenye matibabu, wakati kipa Meyiwa aliuawa kwa kupigwa
risasi Jumapili mjini Vosloorus.
Post a Comment