Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Meya wa jiji la Mbeya Atanas Kapunga wa kwanza kulia akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt Nouman Sigalla wa pili pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Ndugu Jema Msuya wakionyesha kadi maalum ya benki ya ATM itakayo tumiwa na Mashabiki wa na wadau wa Mbeya City kuchangia timu yao ambapo hafla hiyo imefanyika leo katika Hotel ya Gr Hotel Soweto Mbeya. 


Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB,Jema  Msuya akizungumza katika hafla hiyo ambapo kubwa aliwataka  mashabiki na wadau wa Mbeya city kujiunga na benki ya posta Tanzania ambapo watapata kadi maalumu ya ATM papo  hapo kadi ambayo itawawezesha kupata huduma zote za kibenki kwa urais zaidi.
Mashabiki na wadau wa Mbeya city
Mkurugenzi wa  Masoko TPB Bw.Deogratius Kwiyuka akizungumzia juu ya faida ya akaunti hiyo maalumu kwa ajili ya mashabiki wa Mbeya City.
Katibu wa Mbeya City Emanuel Kimbe akizungumza katika hafla hiyo ambapo kubwa amewataka wadau na mashabiki wa Mbeya city kuwa wavumilivu katika kipindi kigumu ambacho timu yao imekuwa ikifanya vibaya.
Meya wa jiji la Mbeya Atanas Kapunga
Mwenyekiti wa Mbeya City Mussa Mapunda



Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top