Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dkt Nouman Sigalla. |
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII INAWATANGAZIA WANANCHI WOTE
KUWA KUTAKUWEPO NA KAMPENI YA UTOAJI WA CHANJO YA SURUA-RUBELLA KWA WATOTO
WENYE UMRI WA CHINI YA MIAKA 15, ITAKAYOANZA TAREHE 18 HADI 24 OCTOBA, 2014
KWENYE VITUO VYOTE VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA, SHULENI NA VILE
VITAKAVYOANDALIWA NA HALMASHAURI HUSIKA.
PAMOJA NA CHANJO HII,
WATOTO PIA WATAPATA CHANJO YA POLIO, MATONE YA VITAMINI A PAMOJA NA DAWA ZA
MINYOO AMBAPO KAMPENI HII ITAHUSISHA MIKOA YOTE YA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR
Mratibu wa huduma za Chanjo Mkoa wa Mbeya Japhet Mhaye. |
CHANJO HII NI SALAMA
NA ITAMKINGA MTOTO DHIDI YA MAGONJWA YA SURUA NA RUBELLA NA MADHARA YAKE.
CHANJO HIZI ZITATOLEWA
BILA MALIPO. EWE BABA,
MAMA, MLEZI HAKIKISHA MTOTO WAKO ANAPATA CHANJO.
Mwisho
Post a Comment