Duru
zimearifu kuwa mama huyo tayari ameondoka katika nyumba ya familia huku dadaake
Adebayor akiambia radio moja ya mjini Accra kwamba Adebayor ndiye aliyemfukuza.
Lakini
mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya Arsenal anadai kwamba mamaake aliondoka
mwenyewe na kwamba hawana mawasiliano yoyote kati yao kwa kuwa amekuwa akitumia
uchawi kutaka kumuharibia kazi yake.
' Ninawezaje
kuzungumza na mama ambaye yeye na dadaangu wamekuwa wakijaribu
kuniroga''aliwauliza maripota.
Mchezo
wa Adebayor katika kilabu ya Tottenham umeathirika katika kipindi cha miezi
kadhaa iliopita huku Tottenham ikidaiwa kujaribu kumuuza kwa mkopo mchezaji
huyo katika dirisha la uhamisho mnamo mwezi January kufuatia kushuka kwa mchezo
wake. CHANZO BBC SWAHILI
Post a Comment