Na Emanuel Madafa,Mbeya .
KLABU ya timu ya Tanzania Prisons imekataa ofa ya kuwauza
wachezaji wao muhimu wawili Nurdin Chono
na Salum Kumenya ili kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania.
Viungo hao wawili wa ushambuliaji wamekuwa gumzo ndani ya
jiji la mbeya kuwa huenda wakanyakuliwa na wekundu wa msimbazi Simba kupitia dirisha dogo.
Akizungumzia hilo,
Katibu wa klabu ya timu ya Prisons, Oswald Morris alisema kikosi cha timu hiyo bado
kinawahitaji wachezaji hao muhimu ili kuisukuma timu hiyo kusonga mbele tofauti
na Simba wanavyofikiria.
Amesema, wiki iliyopita uongozi ullipokea simu kutoka kwa
uongozi wa Stendi United, ukimtaka mchezaji Ibrahim Mamba lakini hakuna barua
iliyowasilishwa mezani.
“Prisons imekuwa ikiingia mkataba na wachezaji kwa miaka
miwili hivyo mpaka sasa tunazaidi ya mwaka mmoja wa kuwamiliki wachezaji wetu,”alisema.
Hata hivyo, Katibu huyo alisema kuwa kikosi cha Prisons
kikiwa na wachezaji wake wote, kinatarajia kuingia kambini November 23 mwaka
huu.
Mwisho.
Post a Comment