Polisi waliojihami wanaendelea kushika doria katika barabara za mji wa Mombasa Pwani ya Kenya hata baada ya maombi ya Ijumaa
Hii ni baada ya vurugu kati ya polisi hao na vijana baada ya kufanya msako katika baadi ya msikiti mjini humo.
Misikiti ambayo ilifanyiwa msako ambako inaaminika mafunzo ya itikadi kali za kidini inafanyika, ni Swafaa na Minaa.
Polisi wanadai kuwa misikiti hii hutoa mafunzo ya itikadi kali ikilenga kuwaunga mkono wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia Al Shabaab.
Vijana waliojaribu kuingia katika msikiti wa Swafaa kwa maombi ya usiku, walikabiliwa na maafisa wa usalama.
Kwa siku nne zilizopita, kumekuwa na hali ya taharuki katika mtaa wa Kisauni baada ya polisi kudfanya msako katika msikiti ya Swafaa na Minaa katika juhudi za kupambana na vijana wenye itikadi kali za kidini na magenge ya vijana wanaowahangaisha wakazi.
Polisi walinasa silaha na vifaa vya kulipua mabomu katika msako huo ulioanza Jumatatu huku zaidi ya watu 100 wakikamatwa kwa madai kuwa walikuwa wanapokea mafunzo ya itikadi kali za kidini huku wakijiandaa kujiunga na kundi la Al shabaab.
Polisi hawajawaruhusu watu kuingia katika misikiti hiyo, na polisi wanasema yeyote atakayekwenda kinyume ya hilo, atakabiliwa na tisho la kupigwa risasi.
Post a Comment