Na Mwandishi wetu,Tanga
TIMU ya Coastal Union ya Vijana U-20 imepania kuhakikisha inatetea
taji lake wanalolishikilia la Michuano ya Kombe la Uhai kwa kufanya vizuri
katika mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni hapa nchini.
Coastal Union U-20 ambao ni mabingwa wa kombe hilo mara baada ya
kuifunga Yanga kwenye mechi ya Fainali ya Mashindano hayo msimu uliopita kwenye
mchezo fainali ambao ulichezwa uwanja wa Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo,Meneja wa timu hiyo,Abdul Ubinde alisema kuwa
maandalizi ya timu hiyo kuelekea michuano hiyo yanaendelea vizuri ambapo timu
hiyo inaendelea na mazoezi yake kila siku kwenye uwanja wa soka Disuza asubuhi
na jioni chini ya Kocha wake,Joseph Lazaro ambaye amepania kutetea taji hilo.
Ubinde amesema kuwa kwenye mashindano hayo msimu huu timu hiyo
itaingia ikiwa na lengo moja la kuhakikisha wanapambana kufa na kupona ili
kuweza kuendeleza kushikilia ubingwa wake kwa sababu ya uimara wa kikosi hicho.
Amesema kuwa hatuendi
kushindana kwenye michuano hiyo bali kuhakikisha tunatetea taji letu la Ubingwa
wa Michuano hiyo ambao sisi tunaingia kama mabingwa watetezi.
Ameongeza kuwa kikosi
cha timu hiyo kimeimarika vilivyo na kipo tayari kushiriki mashindano hayo kwa
mafanikio kutokana na kuwa na wachezaji mahiri wenye uwezo wa kuleta mapinduzi
kwenye michuano hiyo.
Kikosi hicho kinaundwa
na wachezaji nguli akiwemo mlinda mlango namba mbili wa kikosi cha Coastal Union inayoshiriki ligi
kuu Fikirini Suleiman “Mapara”Mohamed Twaha “Dijong”,Mtenje Albano na Mohamed
Omari “Hungry”
Meneja huyo amesema
kuwa wachezaji wa timu hiyo wapo kwenye morali wa kuhakikisha wanafanya vizuri
kwa kucheza kwa umakini mkubwa lengo likiwa kupata matokeo mazuri kila mechi
watakayocheza.
Post a Comment