Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
.
Na EmanuelMadafa,Mbeya 
WANANCHI wa Kijiji cha Ngyekye Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, wamejikuta wakitafuna kitoweo cha nyama ya mbwa baada ya kuuziwa mishikaki kutoka kwa mfanyabiashara Ahadi Jesikaka(20).

Tukio hilo limetokea Nov4 mwaka huu  majira ya saa saba za mchana, katika kijiji cha Ngyekye Kata ya Matema Wilayani Kyela.

Wakizungumza na blog hii  kwa njia ya simu muathirika wa tukio hilo, Anyandwile Mbwilo, alisema hali hiyo imetokea baabda ya kufika kwenye kibanda cha mfanyabiashara huyo na kuagizia chakula kilichoambatana na nyama iliyotengenezwa mithili ya mishikaki.

“Nilifika kwenye kibanda cha chakula kinachomilikiwa na Jesikaka na kuagiza chipsi zilizoambatana na mishikaki baada ya kumaliza kula nilimsikia mmiliki huyu akitoa kauli za ajabu, akidai kwamba “Eti mnajidai hamli mbwa mbona leo mmekula”alisema .

Amesema, baada ya kusikia kauli hiyo yeye pamoja na baadhi ya wateja wa;liokuwa kwenye kibanda hicho , walianza kuhamaki kasha kumtafuta mwenyekkiti wa eneo hilo kwa lengo la kumkamata muhusika huyo na kumshitaki polisi.

Aidha, imeelezwa kuwa awali muhusika huyo, alipohojiwa kwamba ni kweli nyama hiyo ilikuwa ya mbwa, inadaiwa kwamba alikiri lakini hakueleza sababu iliyompelekea kuuza nyama hiyo.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapo kamilika.


Kamanda Msangi, amewataja baadhi ya watu waliodaiwa kuuziwa kitoweo hicho ni Enock Nsemwa(52) mkazi wa Ngyekye na Anyandwile Mbwilo (29) wote wakazi wa kijiji hicho na kwamba ameihasa jamii kuwa makini hususani wanaponunua vyakula ili kujiepusha na madhara ya kiafya.

Mwisho.




Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top