Hoteli
hiyo inatoa huduma kama vile vidimbwi vya kuoga vya wanyama hao,vyumba vyenye
hewa safi na vyakula vya kuvutia, na hivyobasi kuimarisha viwango vya
kuwabembeleza wanyama hao katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa.
Hoteli
hiyo yenye urefu wa futi 4,317 kwa jina Wagington Hotel imejengwa katika nyumba
za zamani za wakolini wa Uingereza zilizobadilishwa katika makaazi ya
wanadiplomasia.
Vyumba
vya kulalia katika hoteli hiyo vinagharimu dola 271 kwa mbwa watatu wanaotumia
kwa pamoja chumba cha kifalme,kilicho na maeneo ya kifahari ya kuweka
balbu,runinga,na vitanda vilivyotengezwa na ngozi.
Hoteli
hiyo iliojengwa hususan kwa mbwa pia huwakaribisha paka.
''iwapo
tunajitakia mema katika maisha yetu, kwa nini marafiki zetu walio waaminifu nao
tusiwafanyie mambo mazuri'' aliuliza mmiliki wa hoteli hiyo Estelle Taylor.
''Kama
watu tunaowapenda wanyama,tuna hisi kwamba ni vyema kuwa na eneo ambalo wanyama
wanaweza kuwekwa ili nao wajisikie nyumbani'' aliongezea.
Wanaomiliki
wanyama hao pia wanaweza kupata eneo la kufanya mafunzo,kunyoa, kukata
kucha,kubadilisha rangi za wanyama hao pamoja na masaji.
Hoteli
hiyo pia hutoa huduma ya gari la kifahari aina ya Limousine kwa wanyama hao
kutoka makaazi yao hadi hoteli hiyo na kutoka hoteli hiyo hadi makaazi yao.
Nchini
Singapore kuna zaidi ya maduka 250 ya wanyama, mengi yakiwa katika maduka
makubwa ya jumla.
Mfanyibiashara
mmoja hutoa huduma za kitalii kila wikendi ambapo wamiliki wa wanyama hao na
wanyama wenyewe hutembezwa katika maboti.BBC SWAHILI







Post a Comment