Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya , imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa askari wa jeshi la polisi askarF 5842 DC Maduhu,  baada ya kupatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia na kuwachilia huru wengine ambao ni E7769 DC Shabani na WP 6545DC Neema.
Askari Maduhu pamoja na wenzake wawili ambao ni  E 7769 DC Shaban na WP 6545 DC Neema  ambao kwa pamoja walikuwa wakabiliwa na kesi  kumuua Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha TEKU Daniel Mwakyusa Februari 14 mwaka 2012 .

Hukumu hiyo ya kesi namba 16 ya mwaka 2013 imetolewa (Nov 19) na jaji Rose Temba baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili.

Awali ilielezwa mahakamani hapo na mawakili wa serikali Archiles Mulisa akisaidiwa na Catherine Paul kuwa washitakiwa walifanya mauaji ya kukusudia mnamo Februari 14 mwaka 2012 kinyume cha kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo,jaji Temba amesema mshitakiwa namba moja DC Maduhu anahusika moja kwa moja na mauaji hayo kutokana na ushahidi wa kimazingira ikiwamo yeye kuwa mtu wa mwisho kuondoka na marehemu eneo la tukio na kumpeleka kwenye gari,risasi tatu kupungua kwenye bunduki yake na pia kuwa mtu wa mwisho kurejesha silaha kituoni.
mwisho






Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top