![]() |
| Familia ya Bob Marley |
Bidhaa
hizo zitajulikama kama 'Marley Natural' na na zitajumuisha mafuta ya urembo
pamoja na manukato mengine ya wanawake na bidhaa nyinginezo.
Bidhaa
hizo zitatengezwa na kampuni kubwa ijulikanano Privateer Holdings iliyo mjini
Washington Marekani, ikisisitiza kutaka kudumisha kumbukumbu ya mwanamuziki
huyo aliyesifika kote duniani.
Bidhaa
hizo zitauzwa nchini Marekani na kwingineko duniani kunzia mwaka jana.
Mwanawe
Bob Marley, Cedella Marley, alisema hayati babake angekuwa hai angefurahishwa
sana na wazo hilo.
''Babangu angekuwa
na fahari kubwa kuona watu wakitambua uwezo wa kuponya wa Bangi,'' alisema
Cedella.
Mkuu
wa kampuni hiyo, Brendan Kennedy alisema Marley alikuwa mtu ambaye kwa njia
nyingi alisaidia kuanzisha harakati za kupinga juhudi za kuharamisha Bangi
miaka 50 iliyopita.
"Marley
alipenda sana kutumia Bangi na hakuna aliyemshinda kwa hilo duniani kote. ''
Bob Marley alifariki
mwezi Mei mwaka 1981, kutokana na Saratani.Alipenda sana kutumia Bangi kama
sehemu ya imani yake ya Rastafarian na kuunga mkono kuhalalishwa kwake.
Matumizi
ya Bangi kwa ajili ya kujiburudisha yamehalalishwa katika majimbo ya Colorado na
Washington nchini Marekani.
Majimbo
mengine huenda yakaidhinisha matumizi ya Bangi nchini Marekani na mengine
tayari yanaruhusu utumiaji wa bidhaa hiyo kwa sababu za matibabu.cHANZO BBC








Post a Comment