![]() |
| Mshambuliaji wa Mbeya city Deus Kaseke |
Na Emanuel Madafa, Mbeya.
KLABU ya timu ya Mbeya City, imesema bado inamshikilia mchezaji
wao Deus Kaseke na kukanusha madai ya
kwamba mchezaji huyo anatarajiwa kusajiriwa na timu za Simba na Yanga kupitia
dirisha dogo.
Kiungo huyo mshambuliaji wa kikosi hicho cha Mbeya City, hivi karibuni
jina lake limeoneka kuchomoza kwenye vyombo vya habari ikionyesha kwamba
mchezaji huyo anakwenda kwa wekundu wa msimbazi Simba sanjari na mshambuliaji
wa Mtibwa Sugar Ame Ali.
Aidha taarifa hizo zimekuwa zikidai kuwa mchezaji huyo huenda
akamwaga wino katika klabu ya Yanga kwa ajili ya kukipiga katika duru la pili .
Akizungumza na blog hii, Katibu mkuu wa klabu hiyo, Emmanuel
Kimbe, alisema mpaka sasa uongozi huo haujapata
ofa yoyote kutoka kwenye vilabu hivyo.
Amesema, hivyo mchezaji
Deus Kaseke anaendelea kuwa mchezaji halali wa klabu ya Mbeya City lakini
Kimbe, hakuwa tayari kuweka wazi mkataba walioingia na mchezaji huyo.
Katibu huyo ameweka wazi kuwa Mpaka sasa bado klabu hiyo inauhalali wa kuendelea kumtumia
mchezaji Deus Kaseke kwani mkataba wake haujamalizika na pia uongozi haujapokea
ofa yoyote kutoka klabu za Yanga na Simba.
Wakati huo huo, timu ya mbeya city inatarajia kuingia kambini
mwishoni mwa mwezi huu kujiwinda na duru inayofuata ya ligi kuu ya soka ya Tanzania
Bara.
Timu hiyo ambayo itafungua dimba na timu ya Ndanda kutokaa Mkoani
Mtwara, mchezo unaotaraji kupigwa kwenye dimba la kumbukumbu ya hayati Edward
Moringe Sokoine Jijini Mbeya.
Hata hivyo, msimu huu timu hiyo haijafanikiwa kufanya vizuri baada
ya kufungwa michezo minne kwenda sare michezo mitatu na kupata ushindi wa
mchezo mmoja dhidi ya Costunion ya Tanga hivyo kujikusanyia jumla ya pointi 5
ikiwa inaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi kuu.
Mwisho.








Post a Comment