![]() |
| Askofu Mkuu Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mbeya Alinikisya Cheyo |
KANISA
la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi, limesema umefika wakati wa
kuwasilisha mgogoro unaoendelea ndani ya kanisa hilo kwa kamati teule ya
usuluhishi wa migogoro ya kanisa nchini inayoongozwa na Askofu Alex Malasusa.
Mgogoro
huo ambao hivi karibuni ulisababisha baadhi ya waumini na wachungaji wa dhehebu
hilo kuzifunga ofisi za Jimbo huku wakitishia kuchafuka kwa hali ya amani
endapohalmashauri kuu ya jimbo haitamrudisha madarakani aliyekuwa Mwenyekiti wa
kanisa hilo,Nosigwa Buya baada ya kusimamishwa kwa tuhuma zakushindwa kusimamia
matumizi ya fedha, hivyo kuliingizia kanisa hasara ya mamilioni ya fedha.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake leo , askofu Mkuu wa kanisa hilo,
Alinikisya Cheyo, alisema wakati umefika kwa viongozi wakubwa wa kiroho
kuingilia kati mgogoro huo na kuumaliza kuliko kuendelea na mabishano ya pande
mbili ambayo hayafikii muafaka licha ya serikali kuingilia kati.
Amesema,
anatarajia kukutana na kamati hiyo teule ya usuluhishi inayoongozwa na Askofu
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT) Alex Malasusa
pamoja na Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Jaji mstaafu Agustino
Ramadhani kwa ajili ya kuomba ushauri wa nini kifanyike ili kumaliza mgogoro
huo.
Alisema,
wao kama kanisa wamefika mahala wameshindwa kufikia muafa kutokana na
muingiliano wa pande mbili ambazo zimekuwa zikisigana hivyo kulifanya jambo
hilo kuendelea kuwa kubwa na gumu.
Amesema,
baadhi ya wajumbe walikuwa wakionyesha kukubali yaishe kwa kulimaliza suala
hilo kwa kuombana msamaha na kumrudisha Mwenyekiti Buya madarakani lakini
wengine walikubali kumsamehe lakini si kurudi madarakani kwa kiongozi huyo.
Hata
hivyo, Askofu huyo, amekiri kwamba halmashauri hiyo imefikia muafaka wa
kuitisha mkutano mkuu wa Sinodi ifikapo Disemba mwaka huu katika kulitatua
tatizo hilo.
Mwisho.
![]() |
Askofu Alex Malasusa.
|
| Hali ilivyokuwa wiki moja kabla ya askofu cheyo kutoa tamko Makao makauu ya kanisa hilo Jakaranda jijini Mbeya . |








Post a Comment