![]() |
Swala la kuidhinishwa maaskofu wa kike daima huzua mjadalaKanisa la England linatarajiwa kupititsha rasmi sheria itakayo waruhusu maaskofu wa kike kuteuliwa kwanzia mwaka ujao. |
Mapadri wa
kwanza wa kike waliteuliwa 1994, lakini hadi sasa hawajaweza kupata majukumu
makuu kanisani.
Mgawanyiko
unazidi kuonekana katika kanisa la kianglikana kati ya wale wanaosema mchakato
huo unaambatana na imani yao na wale wahafidhina wanaopinga.
Juhudu za
hapo awali za kuwatawaza maaskofu wa kike zilishindwa kunawiri mwaka wa 2012,
baada ya wanachama sita wa kawaida wa kikao cha viongozi, kikao kinachobuni
sheria, kutounga mkono wazo hili la maaskofu wa kike.
'Utamaduni kubadilika'
Kura ya
Jumatatu katika kakao cha viongozi huko church house Westminster itawezesha
kupitishwa kwa muhuri wa mwisho wa sheria hiyo, itakayofuatwa na kupitishwa
katika bunge mwezi Oktoba.
Mwandishi
wa habari wa BBC wa maswala ya kidini Caroline Wyatt alisema kuwa "ni
hatua ya kipekee katika huu mchakato wa muda mrefu lakini ni wazi kuwa ni mfano
wa kihistoria sana na wa muhimu pia "
Maombi ya
nafasi hiyo kutoka kwa wanawake tayari imepokelewa katika dayosisi za
Nottingham na South well, ingawa hakutakuwa na habari zozote hadi Januari 2015
Gloucester,
Oxford na Newcastle pia ni madayosisi ambayo maaskofu wapya wanatarajiwa
kuteuliwa.
Uamuzi huu
umepokelewa vyema na wale waliokuwa wakikampeni kwa muda mrefu, inaonekana kuwa
ni njia nzuri ya kuongeza ushiriki wa wanawake kanisani.
Mchungaji
mkuu Jane Hedges wa Norwich amesema kuwa hapo awali alidhani kuwa mchakato huu
hautafanyika hadi kustaafu kwake.
Alifikiria
kuwa "watu walishangazwa jinsi wanawake wamekubalika kwa haraka kwa kama
mapadri" aliongezea kuwa njia ya kukuwa padri ingechukua muda mrefu.
Kwa sasa
wanawake wanakarabia 35% katika uongozi wa kanisa.
'Sio muafaka'
Katika
mwezi wa Oktoba, kanisa lilisema kuwa ubaguzi chanya unaweza kutumika kuwaweka
maskofu wa kike ambao hawajawakilishwa vizuri.
Askofu
Mkuu wa Canterbury Justin Welby amepongeza kura ya kihistoria iliyofanyika
mwanzoni mwa mwaka huu kama "ni mwanzo wa tukio kubwa linaloweza kushamiri
ama linalotatanisha"
lakini
hatua hii ya kuteuwa maaskofu wa kike haitapokelewa vyema duniani.
Kitengo
kinachopinga mchakato huo - the conservative evangelical group Reform -
wanasisitiza kuwa "amri ya uongozi wa kiume katika kanisa inakataza
wanawake kuwa viongozi katika madayosisi"
Mageuzi
haya yanakadiria kuwa robo ya makanisa itapata kuwa hayambatani na imani zao.
Sheria hii
inajumuisha miundo ya kusimamia watu wenye maoni tofauti kwa mfano kubuni
wakaguzi huru watakaosimamia mipangilio ya parokia zinazohitaji uangalizi wa
Maaskofu wa kiume.







Post a Comment