Na Mwandishi wetu,Mbeya
Wachezaji 20 wa mpira wa
kikapu Mkoa wa Mbeya, wanatarajia kushiriki mashindano ya Taifa CUP,
yatakayofanyika Mkoani Dodoma November
23 hadi November 30 mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kupokea Katibu
wa timu hiyo, Yusuf Nyirenda, alisema kuwa wanawashukuru Coca Cola kwa
kuchangia kiasi hicho cha fedha .
"Kwa kushirikiana na Coca Cola,
tunaamini kuwa mpira wa kikapu utapata msukumo mkubwa na kupiga hatua zaidi
nchini lakini bado tunakabiliwa na changamoto ya kifedha,” alisema Nyirenda.
Alisema, timu inatajia kuondoka Mbeya
November 20, ikiwa na wachezaji 20 kati yao wanawake 10 na wanaume 10 lakini
mpaka sasa wamefanikiwa kupata shilingi milioni moja kati ya milioni
4,700,000 zinazohitajika.
“Kiasi cha shiringi milioni 4,700,000
kinahitajika kwa ajiri ya usafiri wa kwenda na kurudi, chakula, malazi na ada
ya kushiriki mashindano haya,”alisema.
Alisema, gharama hizo ni kwa wachezaji 10
wanaume ,wanawake 10 na viongozi wawili ambao wataondoka na timu hiyo lakini
bado timu inauhitaji wa shilingi milioni 3,600,000 hivyo kuwaomba wadau
kujitokeza kuichangia timu hiyo ili iweze kushiriki..
Meneja kutoka Kampuni ya
vinywaji baridi ya Coca Cola Haji Ally , alisema wanajua kuwa mashindano ya mwaka
huu yatashirikisha mikoa mbalimbali hivyo
wametoa kiasi hicho cha fedha katika kuisaidia timu ya Mbeya
kushiriki mashindano hayo.
Hata hivyo, aliwaomba wadau na
mashabiki wa mpira huo, kujitokeza kwa wingi katika kuichangia timu hiyo ili
iweze kufika Mkoani Dodoma na kushiriki mashindano hayo.
Mwisho.






Post a Comment