KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA AHMED .Z. MSANGI-SACP
ANAWATANGAZIA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014 NA KIDATO CHA NNE MWAKA
2013 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI BAADA YA USAILI KUKAMILIKA
Maelekezo
Muhimu.
- Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014, kidato cha nne
mwaka 2013 na JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo, Bulombola, Kanembwa,
Itende, Nachingwea, Mbweni, Maramba, Chita, Makutupola, Mtabila, Msange,
Mgulani, Oljoro, Rwankoma na Kimbiji wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya
awali ya Jeshi la Polisi.
- Wahitimu hawa waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti tarehe
28/11/2014 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kama ilivyooneshwa kwenye
jedwali hapa chini ili waandaliwe usafiri wa kuwapeleka Shule ya Polisi
Tanzania tarehe 30/11/2014.
- Zoezi la usajili litaanza shuleni hapo tarehe
01/12/2014 hadi tarehe 15/12/2014. Atakaefika kuanzia tarehe 16/12/2014
hatapokelewa.
- Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako
hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Shule ya Polisi Tanzania
mjini Moshi.
- Vijana hawa watalazimika kufika shuleni wakiwa na
mahitaji yafuatayo:
- Vyeti vyao vyote vya masomo( original Academic
Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha
Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth certificates). Hati ya kiapo
cha kuzaliwa haitakubalika.
- Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)
- Chandarua chenye upana futi tatu
- Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)
- Pasi ya Mkaa
- Ndoo moja
- Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingi elfu
hamsini na mia nne tu (50,400/=).
- Pesa kidogo ya kujikimu.
- Kwa mujibu wa kanuni za shule ya Polisi ni marufuku
kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakayepatikana na simu atafukuzwa
shuleni hapo. Shule itaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano.
- Angalia orodha kwenye tovuti ya www.policeforce.go.tz au fika
Ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya iliyopo Forest barabara ya
mahakama kuu.
/////////////////////////////////////////////////////////////MWISHO////////////////////////////////////////////////////
Post a Comment