Baadhi ya wamachinga waliobolewa maeneo yao wakijaribu kuambulia japo misumali tu na nondo |
Hawajui chakufanya |
Na Emanuel Madafa Mbeya
Wafanyabiashara
ndogondogo ‘Machinga’ waliovamia eneo la
NaneNane lililopo Jijini Mbeya na kujenga vibanda vyao, jana walijikuta
kwenye wakati mgumu baada ya halmashauri ya Jiji kuvibomoa vibanda hivyo
kutokana na kujengwa kinyume cha sheria.
Eneo hilo , lilitengwa na halmashauri ya Jiji la Mbeya, kwa ajili
ya kuwaweka wamachinga zaidi ya 800 waliokuwa wakiendesha shughuli zao kwenye
maeneo ambayo yaliyopigwa marufuku, pamoja na wale waliondolewa kwenye eneo la
Soko la Mwanjelwa baada ya kuungua moto mwaka 2006.
Katika operesheni hiyo,vibanda zaidi ya 150 vimebomolewa na watendaji wa halmashauri hiyo na kwamba zoezi hilo lilikuwa likiendeshwa chini ya Mwanasheria wa Jiji la Mbeya, Crispin Kaijage.
Kabla ya uongozi wa Jiji, kufikia uamuzi wa kubomoa vibanda hivyo, Baraza la Madiwani lililoketi November 21 mwaka huu, kupitia wajumbe wake, walitaka kufahamu utaratibu uliotumika wakati wa ugawaji wa eneo hilo baada ya kupokea malalamiko ya kwamba eneo hilo limegaiwa kwa wafanyabiashara wakubwa.
Kutokana na kauli hiyo, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, alimtaka Mkuu wa idara hiyo Vicent Msola kujibu malalamiko hayo, ambaye alikiri wazi kwamba eneo hilo limevamiwa na watu ambao hawakuwa walengwa.
Mwisho.
Post a Comment