Na Ezekiel Kamanga,Mbeya
Wakati Asasi ya TGNP,TAMWA na nyinginezo zikipaza sauti kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya watoto na wanawake bado vitendo hivyo vimeendelea kushamiri shule ya msingi Iwalanje Kata ya Ijombe Wilaya ya Mbeya Mkoani Mbeya.
Tukio la hivi karibuni lililofanya nishindwe kujizuia kutoa machozi baada ya kupata taarifa kutoka kwa mwanaharakati wa kupinga vitendo vya kikatili Yassin Yuta mkazi wa Ijombe iliazimu kufika eneo hilo na kushuhudia ukatili huu ambapo watoto wa darasa la nne hadi la sita walikuwa wakibebeshwa tofali nne kila mmoja muda wasomo bila kujali jinsia na umri.
Tofali hizo zilikuwa zikitolewa eneo moja kwenda jingine umbali wa kilometa moja huku baadhi ya watoto wakilia kutokana na uzito wa tofali hizo na walikuwa wakisimamiwa wakisimamiwa na mwanafunzi mwenzao aliyekuwa akihakiki kwa kuorodhesha majina kwenye daftari.
Hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa wanafunzi hao walikuwa wakifanyishwa kazi na mwalimu wao aliyefahamika kwa jina moja la mwalimu Nyoni na tofali kupelekwa kwenye nyumba ya mkazi mmoja wa Kijiji cha Nsalaga Jijini Mbeya ambaye alifahamika kwa jina moja la Simbengale ambapo inadaiwa kumlipa mwlimu huyo ujira huku wanafunzi hao wakiambulia patupu.
Aidha mtendaji Kata aliyefahamika kwa jina la Zawadi Mbembela alikiri kupokea taarifa hizo na kuahidi kufuatilia.
Baadhi ya wazazi wamedai kuwa watoto wao wamekuwa wakitumikishwa na baadhi ya walimu hao muda wa masomo na hivyo watoto wao kushindwa kupata haki yao ya elimu.
Wamemtaka Afisa elimu Wilaya kutembelea shule hiyo kutokana na Mratibu wa elimu kushindwa kuchukua hatua dhidi ya watoto hao.
Wilaya ya Mbeya Vijijin inakabiliwa na ukwasi wa fedha kitengo cha ukaguzi na baadhi ya shule hazijakaguliwa kwa zaidi ya miaka nane na walimu kutumia mwanya huo kuwatumikisha wanafunzi.
picha zote na Ezekiel Kamanga
Post a Comment