Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abas Kandoro
Na  Mwandishi wetu
SERIKALI Mkoani Mbeya, imelazimika  kukifunga kiwanda cha Bale Fruits&Beverages Enterprises kinachozalisha bidhaa aina ya juice kwa muda usiojulikana kutokana na kukiuka  taratibu za uzalishaji.

 Bidhaa zinazo tengenezwa na kiwanda hicho bubu zimekuwa z imekuwa zikiuzwa kwa shilingi 300 hadi 400  kwa watumiaji ambao asilimia kubwa ni watoto.


Kiwanda hicho  kilichopo katika eneo la Itiji lililopo Jijini Mbeya, kimekuwa kikizalisha bidhaa hiyo ya juisi maharufu ikiwa na nembo ya biashara “Halisi Orange Drink” na kuisambaza kwa walaji waliomo ndani ya Jiji la Mbeya na Mkoa wa jirani wa Ruvuma.

Akizungumzia  uamuzi wa kukifunga kiwanda hicho, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro, amesema serikali ilipokea taarija ya uwepo wa kiwanda hicho na  tayari imetoa maelekezo kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa kukifunga haraka iwezekanavyo.

Kandoro, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya, alisema serikali hairuhusu mtu yoyote  kuanzisha kiwanda bila ya kufuata taratibu za kisheria hivyo ni vema kiwanda hicho kikafungwa ikiwa na kukamatwa kwa mmiliki huyo.

Akizungumzia sakata hilo, Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nyanda za Juu Kusini, Rodney Alananga, alikiri  kupokea taarifa hiyo na kuifanyia kazi kwa kukifunga kiwanda hicho na kuthibitisha kwamba bidhaa hiyo si salama kwa afya ya mlaji kutokana na kutokaguliwa na TBS.

Alisema, November 7, mwaka huu timu ya TFDA ikiongozana na wataalamu kutoka halmashauri ya Jiji la Mbeya ilifika katika eneo la tukio na kujionea hali halisi  ya mazingira ya kiwanda hicho kwamba si rafiki hivyo kuamuru kufungwa kwa kiwanda hicho.

Aidha, Alananga  alishindwa kuweka bayana hatua zilizochukuliwa na uongozi huo katika kudhibiti  bidhaa ambayo tayari imeingia sokoni na walaji wameendelea kuitumia.

Hata hivyo, akizungumzia tuhuma hizo mmiliki wa Kiwanda hicho, Jonas Bushambali, kwa njia ya simu, alisema yeye yupo njiani anaelekea Jijini Dar es Salaam na kuwataka waandishi wa habari kuonana naye siku ya Jumanne ya wiki ijayo kwani hawezi kulizungumzia suala hilo kwa njia ya simu.

Akizungumzia madhara yatokanayo na bidhaa hiyo  kwa  walaji, Mganga Mkuu wa halmashauri ya Jiji la Mbeya, Samweli Lazalo, alisema walaji wapo hatarini kukumbwa na homa za matumo kutokana na bidhaa hizo kuzalishwa chini ya kiwango na katika mazingira machafu.

Mbali, na homa za matumbo, pia Lazalo akiri wazi kwamba kutokana na bidhaa hiyo kutokaguliwa  hivyo kiwango cha kemikali kilichotumiwa ndani hakijulikani .

Bidhaa inayotengenezwa na kiwanda hicho.
JAMIIMOJABLOG

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top