Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Baadhi ya wanafunzi wa chuo  cha Mchepuo wa Kilimo cha Nice Dream, kilichopo Jijini Mbeya, wakiwa katika chumba cha darasa wakiwa hawajui hatima ya maisha yao mara baada ya uongozi wa chuo hicho kuwatelekeza wananfunzi hao wa


Jiwe la Msingi linalo onesha kuwa limefunguliwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Fredrick Sumaye ambapo kwa muibu wa wanafunzi wanaosoma chuo hicho walidai kuwa wao ndio walioandika jina kwa kulazimishwa na walimu wao.





Bweni linalokaliwa na wanafunzi wa kiume 


Hapa Ndipo wanapo lala wanafunzi hawa








Muda wa chakula ambapo huo ni wamara moja tu kwa siku na mwendo wa kabegi na Nguna yani ugali







Hili ndilo bweni la wasichana na ni sehemu ya kulia chakula.soma habari kamili 
NaMwandishi wetu,Mbeya
SERIKALI  Wilayani Mbeya, imefikia uamuzi wa kukifunga chuo cha Mchepuo wa Kilimo cha Nice Dream, kilichopo Jijini Mbeya, baada ya uongozi kuwatelekeza wananfunzi wa chuo hicho pamoja na kufanikiwa kuondoka na mamilioni ya fedha yaliyotokana na ada za watoto hao.

Chuo hicho ambacho kinasemekana hakitambuliwi na serikali kilianzishwa mwezi September mwaka huu katika mtaa wa Mapelele Kata ya Ilemi iliyopo ndani ya Jiji la Mbeya kikiwa na wananfunzi 48.

Hata hivyo, imeelezwa kwamba mbali na wananfunzi hao kutapeliwa fedha zao, pia wamekuwa wakiishi kwa kusaidiwa chakula na majirani wanaokizunguka chuo hicho.

Akizungumzia sakata hilo, Diwani wa Kata hiyo, Furaha Mwandalima, alikiri uwepo wa chuo hicho na kudai kuwa yeye alipokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanachuo ambapo alifika kwenye eneo la tukio na kujionea hali halisi.

Aidha, amesema kuwa baada ya kuona hali hiyo, alitoa taarifa kwa uongozi wa juu ambao walitoa maelekezo yaliyowataka wanafunzi hao kujihoredhesha majina yao ili serikali iangalie utaratibu wa kuwarudisha makwao na Chuo kifungwe.

Amesema, kwa mujibu wa taarifa aliyoipata ni kwamba wanafunzi 42 wanatokea Mkoa wa Kagera na wawili wakitokea mkoani Mara ambapo wawili wanatokea wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya hali mmoja akitokea Mkoa wa Dar es Salaam.

Mmoja wa wanachuo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema waliletewa taarifa na wakuu wa shule walizokuwa wakisoma baada ya kumaliza kidato cha nne mwaka uliopita kuwa wamechaguliwa na serikali kusomea Kilimo Mkoani Mbeya lakini walipofika walishangazwa na hali waliyoikuta na kwamba walipofuatila kwenye mtandao walibaini chuo kutosajiliwa katika Baraza la Vyuo.

Walipoutafuta uongozi wa Chuo hicho ulianza kupiga chenga ndipo walikwenda kutoa taarifa Polisi na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambapo uongozi wa Wilaya umeanza hatua za kumtafuta mmiliki ili aweze kutoa majawabu.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, alisema askari wa kitengo cha upelelezi wanafuatilia suala hilo ili kuwatia nguvuni wahusika na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Hata hivyo, aliwashauri wanafunzi hao kuanza kutafuta njia mbadala ya kujiendeleza kielimu kwa kutafuta vyuo vingine kuliko kuendelea kupoteza muda wao wakiendelea kuwasubili wahusika hao ambao mpaka sasa hawajulikani walipojificha.


Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top