Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Meneja Mkuu wa Pepsi Ndugu Sanjay Monshi akizungumza katika uzinduzi huo ambao umefanyika katika kiwanda cha Pepsi Iyunga jijini Mbeya.


Meneja Mauzo Kampuni ya vinywaji baridi vya Pepsi Ndugu Ommary Jumbe akizungumzia lengo la shindano hilo.


Afisa Rasilimali watu Kampuni ya Pepsi Ndugu Edwin Arbogast







Na Emanuel Madafa,mbeya
Kampuni ya SBC Tanzania Limited Watengenezaji na wasambazaji  wa vinywaji baridi aina ya Pepsi,Mirinda,7up,Mountain Dew na Evervess wamezindua shindano maalum linalojulikana  kama Jishindie Mamilioni kila siku na Pepsi.

 Shindano hilo litahusu Soda aina ya Pepsi ,Mirinda Orange ,Mirinda Fruty,Mirinda Green Apple ,pamoja na MountainDew (300mil) na seven up zenye ujazo wa milimita 350 tu. 

Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja Mkuu wa Pepsi Ndugu Sanjay Munshi amesema shindano hilo litaendeshwa kuanzia Nov 10 hadi Des 21 mwaka huu ambapo litahusisha mikoa ya Dar es salaam,Pwani,Morogoro,,Dodoma,Mtwara,Iringa,Njombe Ruvuma Rukwa na Katavi.ambapo vizibo vya shindano la jishindie Mamilioni kila siku na Pepsi vitakuwa narangi ya dhahabu .

Amesema shindano hilo litakuwa na zawadi na pesa tasilimu kiasi cha shilingi 2,500,000 na ,1,000,000 pamoja na 500,000 huku zawadi nyingine zikiwa ni soda za bure .

Aidha kwa upande wake Meneja Mauzo wa Pepsi Mbeya Ndugu Omary Jumbe amesema  ili mteja ajishindie  zawadi anatakiwa kununa soda za jamii yaP epsi  kisha abandue  ganda ndani ya kizibo ambapo anaweza kukuta maandishi ya viwango hivyo vya feza  au zawadi ya Soda na kubahatika kuibuka mshindi.
mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top