Na Boniface Wambura,Dar es salaam
Kikosi cha wachezaji 23 wa Taifa Stars tayari kimewasili
Johannesburg, Afrika Kusini tayari kwa maandalizi ya mechi dhidi ya Kalenda ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland.
Mechi hiyo itafanyika Jumapili (Novemba 16
mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Swaziland. Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwepo Johannesburg hadi Ijumaa
itakapoondoka kwenda Mbabane.
Wachezaji wote walioitwa na Kocha Mart
Nooij wapo kwenye msafara huo isipokuwa kiungo mshambuliaji Mrisho Ngasa ambaye
amebaki Dar es Salaam kutokana na matatizo ya kifamilia.
Taifa Stars inatarajia kurejea nyumbani Jumatatu (Novemba 17 mwaka
huu) saa 12.45 jioni kwa ndege ya South Africa Airways.
Wakati
huo huo,
kikosi cha maboresho cha Taifa Stars kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya
Taifa ya Rwanda kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 23. Mechi hiyo
itachezwa Desemba 9 mwaka huu nchini Tanzania.
Kikosi cha maboresho cha Taifa Stars
kinachoundwa na wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 kitakuwa kinakutana mara
moja kila mwezi hadi Mei mwakani kwa ajili ya mazoezi na kucheza mechi moja ya
kirafiki.
Kocha Mart Nooij atatangaza kikosi kwa
ajili ya mechi hiyo na programu nzima mara atakaporejea kutoka Swaziland.
mwisho.







Post a Comment