Na Boniface Wambura,Dar es salaam
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara
inaendelea wikiendi hii ambapo tiketi za elektroniki hazitauzwa tena kwenye
magari, hivyo washabiki wanunue tiketi hizo kwenye mtandao au kwenye maduka ya
CRDB Fahari Huduma.
Kesho (Novemba 8 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam kutakuwa na mechi kati ya Yanga na Mgambo Shooting
wakati Uwanja wa Chamazi kutakuwa na mechi kati ya Azam na Coastal Union.
Jumapili ni mechi kati ya Simba na Ruvu Shooting.
Viingilio kwenye mechi za Uwanja wa Taifa
ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, sh. 8,000 (viti vya rangi ya
chungwa), sh. 15,000 (VIP B na C) wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Mechi za
Uwanja wa Chamazi kiingilio ni sh. 3,000 kwa sh. 10,000.
Mechi nyingine za VPL kesho ni kati ya Stand United na Mbeya City
(Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), Mtibwa Sugar na Kagera Sugar (Uwanja wa
Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo ya saba itakamilika Jumapili kwenye Uwanja wa Chamazi,
Dar es Salaam kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Ndanda kutoka Mtwara.
Wakati huo huo, mchezaji bora wa VPL kwa
mwezi Oktoba, Salum Abubakar wa Azam atakabidhiwa zawadi yake kesho (Novemba 8
mwaka huu) kabla ya mechi kati ya Azam na Coastal Union.







Post a Comment