![]() |
| Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo Ndugu Nicolaus Fungo akiwa akiendelea kupatiwa matibabu katika hospital ya Rufaa Mbeya ambapo hali yake inaendelea vyema baada ya kuapitiwa matibabu. |
Watu37 wamejeruhiwa mara baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka mkoani Mbeya kwenda Dar es salaam kupasuka
tairi na kupinduka katika eneo la Meta, Chimala, Mbarali mbeya.
Ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Happy Nation lenye namba za
usajili T. 281 ARR Scania lililokuwa likendeshwa na dereva aliyefamika kwa jina
moja la Shabani.
Taarifa iliyothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Ahmed
Msangi inasema kuwa basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mbeya kuelekea mkoani
Dar es Salaam.
Amesema ajali hiyo imetokea leo Nov 7 majira ya asubuhi baada ya kupasuka tairi la
mbele kushoto hali ambayo ilisababisha kuacha njia na kupinduka.
Amesema mara baada ya kupasuka tairi dereva alishindwa kuimudu nahasa
kutokana na eneo lenyewe kuwa na kona kali hivyo aliamua kuligongesha kwenye
ukingo wa barabara nakusabisha hali hiyo.
Aidha Msangi
amesema kuwa kati ya majeruhi hao 29 ni wanaume na wengine 8 nakwamba hakuna mtu
aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.
Amesema kuwa majuruhi Sita kati ya wote hali zao ni mbaya na tayari
wamefikishwa katika hospitali ya rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi wakati majeruhi
wengine 10 wakiwa wanapatiwa matibabu katika kituo cha afya Chimala.
Akithibitisha kupokea kkwa majeruhi hao Muuguzi katika chumba cha
msaada wa haraka hospitali ya Rufaa Mbeya Dkt Orivia Masoi amesema kuwa wamepokea
majeruhi sita ambapo wanne wamelazwa wodini na wawili tayari wameruhusiwa.
Aidha mmoja wa majeruhi Nicolaus Fungo ambaye amelelazwa wodi namba moja kwa ajili ya
matibu hao amesema majeraha makubwa maeneo ya mbavuni na kwamba hali yake
inaendelea vizuri mara baada ya kuaptiwa matibabu.










Post a Comment