| Wafanyakazi wa mamlaka ya Mapato TRA Mbeya wakishusha moja ya vitu vilivyotolewa msaada katika gereza la watoto watukutuku Kabwe Mbeya. |
| Meneja wa TRA Mbeya Anord Maimu akikabidhi msaada kwa mmoja wa maafisa usatwi wa jamii wanaotoa huduma katika gereza hilo Bi.Devotha Nicolaus. |
| Afisa ustawi wa jamii Bi.Devotha akishukuru kwa kupokea kwa huo.a msaada |
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),leo Novemba 19,2014 wametembelea Kituo cha watoto yatima pamoja na gereza la Watoto watukutu lililopo Kabwe jijini hapa na kutoa misaada ya mahitaji mbalimbali vyenye vinavyokadiliwa kuwa na thamani ya shilingi Laki 7
Aidha Msaada huo umegaiwa katika kituo cha kulelea watoto yatima
cha Nuru Opharns Center cha Uyole pamoja na Gereza
la watoto watukutu lilopo eneo la Kabwe jijini hapa.
Akikabidhi msaada huo Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA)Mkoa wa
Mbeya Ndugu Anord Maimu amesema utaratibu huo ni mpango enedelevu uliowekwa na
mamlaka hiyo kila mwaka katika muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya
Mlipa kodi .
Amesema msaada huo ambao ni mahitaji muhumu unatokana na
michango ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo ambao wameguswa moja kwa moja kutokana
na uhitaji wa msaada huo .
Amevitaja vitu vilivyotolewa
na mamlaka hiyo kuwa ni pamoja na Mchele ,
sabuni , mafuta ya kula sabuniya unga sukari
na madaftari.pamoja na juice na dawa za meno.
Kauli mbiu ya mwaka huu "Risiti ni Haki
Yako,Unaponunua Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti" ambapo
kilele chake kwa mkoa wa mbeya anatalajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas
Kandor Novemba 21,2014 katika viwanja vya ukumbi wa mkapa jijini hapa.
Mwisho.
| Wafanyakazi wa TRA Wakiwa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru Orphans Center kilichopo uyole katika jijini hapa. |
| Mama Mlezi wa kituo hicho Bi.Amanda Fihavango |






Post a Comment