Gharama za unene wa
kupitiliza duniani ni karibu sawa na utumiaji wa bidhaa za tumbaku ukiwemo
uvutaji wa sigara au sawa na gharama za vita na kubwa kuliko unywaji wa pombe
au mabadiliko ya tabia nchi, unasema utafiti.
Taasisi ya The
McKinsey Global Institute imesema inagharimu pauni za Uingereza trilioni £1.3,
au asilimia 2.8% ya shughuli ya kiuchumi kwa mwaka - inagharimu pauni za
Uingereza bilioni £47.
Watu wapatao bilioni
2.1 - kiasi cha asilimia 30% ya idadi ya watu duniani- wana uzito wa kupita
kiasi au wana vitambi, watafiti hao wamesema.
Wamesema hatua ambazo
ni wajibu wa mtu binafsi, zinatakiwa kutumiwa ili kutatua tatizo hili.
Ripoti hiyo inasema
kuna "gharama kubwa za kiuchumi", na uwiano unaweza kukua kufikia
karibu nusu ya idadi ya watu duniani ifikapo mwaka 2030.
Gharama ya fedha kwa
wenye vitambi inazidi kuongezeka- kwa huduma za afya na kwa upana zaidi katika
uchumi. Kwa kusababisha maradhi, kitambi kina madhara katika utendaji wa kazi
na kupotea kwa tija.
Watafiti wanasema kuwa
sera zenye mwelekeo zinahitajika kufikiriwa.
Dr Alison Tedstone,
mkuu wa masuala ya lishe katika Public Health England (PHE), amesema:
"Ripoti hiyo ni mchango mzuri katika mjadala wa vitambi. PHE imesema
ujumbe wa elimu pekee haisaidii kutatua tatizo la unene wa kupitiliza."
Dr Tedstone amesema
unene wa kupita kiasi unataka hatua za kitaifa na serikali za mitaa, viwanda na
jamii kwa ujumla, na hakuna jibu moja katika kukabiliana na hali hiyo".BBC SWAHILI
Post a Comment