Jumma Mwambusi |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Siku chache, baada ya kocha, Juma Mwambusi kutangaza kujiuzulu, kumeibuka tetesi kwamba huenda
kocha huyo akarejea tena ulingoni kukinoa kikosi hicho endapo uongozi utaridhia baadhi ya masharti aliyoyapendekeza kocha huyo.
Taarifa za ndani zilizoifikia Blog hii, kutokaa ndani ya klabu hiyo, zimeweka wazi kwamba, uongozi wa klabu hiyo, umeonyesha imani kubwa na kocha Mwambusi hivyo kumtaka kurejea tena kikosini.
Moja ya masharti ambayo yamewekwa bayana na kocha huyo kwamba ni lazima uongozi kuyatekeleza ni kwamba endapo atarejea kikosini
asingependa uongozi kumuingilia kwenye majukumu yake ya kiutendaji.
Pia uongozi, huo umetakiwa kuweka mipaka kwa mashabiki ambao kwa sasa wameonekana kuitawala klabu hiyo
hadi kufikia hatua ya kuingilia utendaji wa mwalimu kwa kumtaka kupanga wachezaji wanaowataka wao.
Akizungumzia hilo,
Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya
timu hiyo, amesema suala la kocha
kujiuzulu bado linafanyiwa kazi na uongozi na kwamba vikao vya kulijadili
bado vinaendelea kufanyika.
Amesema bado wanaendelea
na vikao vya ndani hivyo suala la kocha
Mwambusi liko mezani nakwamba hivi sasa
ndio wanaelekea kulijadili na kulitolea
tamko kesho Nov 21 katika mara baada ya kukamilika kwa baraza la Madiwani
.Hata hivyo masharti ya kocha huyo yametajwa kuwa huenda yakawagharimu baadhi ya viongozi.
.Hata hivyo masharti ya kocha huyo yametajwa kuwa huenda yakawagharimu baadhi ya viongozi.
Mwisho.
JAMIIMOJABLOG
Post a Comment