Na Boniface Wambura,Dar es salaam
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16 mwaka huu jijini Mbabane.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16 mwaka huu jijini Mbabane.
Akizungumza
Dar es Salaam, leo (Novemba 5 mwaka huu), Nooij alisema kikosi hicho kitaingia
kambini Novemba 10 mwaka huu saa 6 mchana kwenye hoteli ya Accomondia, na siku
hiyo hiyo jioni kitafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana.
Novemba 11 mwaka huu, Taifa Stars inayodhaminiwa
na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka kwenda Afrika Kusini ambapo itaweka
kambi ya siku mbili kabla ya kuondoka Novemba 13 mwaka huu kwenda Swaziland.
Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni
makipa Aishi Manula (Azam) na Deogratias Munishi (Yanga). Mabeki ni Abubakar
Mtiro (Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam), Emmanuel Simwanda (African Lyon),
Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr
Joshua (Yanga), Said Moradi (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari
Kapombe (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Erasto
Nyoni (Azam), Haruna Chanongo (Simba), Himid Mao (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al
Markhiya, Qatar), Said Ndemla (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji ni Juma Luizio (ZESCO,
Zambia), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon
Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo).
Wakati huo huo Michuano
ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayoshirikisha timu 24 katika makundi manne ya
timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini inaanza kutimua vumbi Novemba
22 mwaka huu ambapo Mpanda United itakuwa mwenyeji wa Ujenzi Rukwa.
Mechi hiyo ya kundi A itachezwa kwenye Uwanja wa
Mandela mjini Sumbawanga. Siku hiyo hiyo katika kundi hilo kutakuwa na mechi
kati ya Mvuvumwa FC na CDA (Lake Tanganyika, Kigoma), na Milambo dhidi ya
Singida United kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Kundi B mechi za ufunguzi ni kati ya Pamba na JKT
Rwamkoma kwenye Uwanja wa CCM Kirumba huku Bulyanhulu FC ikiwa mwenyeji wa AFC
kwenye Uwanja wa Bulyanhulu mkoani Shinyanga.
Abajalo FC ya Dar es Salaam itaikaribisha Kariakoo FC
ya Lindi kwenye mechi ya kundi C itakayochezwa Uwanja wa Karume. Nazo Kiluvya
United na Transit Camp zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo
Mlandizi mkoani Pwani.
Kundi D
mechi tatu za ufunguzi ni kati ya Town Small Boys na Volcano FC (Uwanja wa
Majimaji, Songea), Njombe Mji na Mkamba Rangers (Uwanja wa Sabasaba, Njombe),
na Wenda FC dhidi ya Magereza Iringa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.







Post a Comment