Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Rais Uhuru Kenyatta mara ya mwisho alipokuwa katika mahakama ya ICC
Mahakama ya kimataifa ya ICC imetupilia mbali kesi ya jinai inayomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Mwendesha mkuu wa mashitaka Fatou Bensouda ameondoa kesi dhidi ya Kenyatta ambaye alidaiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007/2008.
Mahakama ilikuwa imempa Bensouda wiki moja kuamua ikiwa ataendelea na kesi dhidi ya Kenyatta au la.
Kenyatta alishtakiwa kama mshukiwa mkuu wa ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/2008 akituhimiwa pamoja na William Ruto ambaye ni naibu Rais.BBC SWAHILI

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top