Na EmanuelMadafa,Mbeya
Baada
ya kumaliza na kufanikiwa kumrudisha kocha wake, Jumma Mwambusi aliyetishia
kuondoka katika klabu hiyo kutokana na matokeo mabaya, klabu ya Mbeya City imefanikiwa kumsajili
beki kisiki Jumma Nyoso.
Kabla
ya kutua Mbeya City, Nyoso alikuwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake
na nyingine ya ligi Kuu ya Coastal Union katika msimu iliopita .
Kusajiliwa
kwa beki huyo kisiki aliyewahi kutamba na timu za Simba na Taifa stars, huenda ikasaidia kuiokoa timu hiyo na matokeo
mabaya iliyoyapata tangu kuanza kwa ligi kuu ya Tanzania Bara, Septemba 20
mwaka huu.
Katika
michezo saba iliyocheza kabla ya ligi kusimama imefanikiwa kushinda mchezo
mmoja tu na sare michezo miwili, huku ikifungwa michezo minne.
Hali
hiyo ilionekana kuwakera mashabiki wa timu hiyo ambayo msimu uliopita ilipata
mafanikio makubwa na kufanikiwa kumaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tatu.
Mwenyekiti
wa Klabu hiyo, Mussa Mapunda, amethibisha klabu yake kumsajili beki huyo na kwamba bado wanaendelea
na mchakoto wa kutafuta wachezaji wengine kadhaa ingawa hakuwa tayari kuweza
wazi kuwa ni akina nani na wanatoka timu gani.
“Nyoso
alikuwa ni mchezaji huru na tayari tumemalizana nae kama ilivyosikia na sisi
tumempa mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya kutusaidia katika michezo iliyobaki
ya ligi ”, alisema Mapunda.
Hata
hivyo habari zilizopo zinadai kuwa klabu hiyo iko mbiuoni kumalizana na
mchezaji mwingine wa kimataifa kutoka nchini Uganda na washambuliaji wawili
kutoka timu kubwa zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara.
Mwisho.







Post a Comment