Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Mtu mmoja mwenye asili ya Kisomali na Kiethiopia ambaye hakuweza kufahamika jina, jinsi ya kiume, mwenye umri kati ya miaka 25-30 amekutwa amekufa vichakani mita tatu kutoka barabara kuu ya mbeya/tunduma

Mwili wa marehemu ulikutwa eneo la Kijiji cha Kilimampimbini, Kata ya Vwawa,  wilaya ya mbozi, mkoa wa mbeya mnamo Desemba  10 mwaka huu  majira ya saa 15:00 alasiri.

Aidha Mwili wa marehemu huyo  umekutwa ukiwa hauna jeraha lolote na ukiwa umedhoofika sana.

Aidha baada ya kupekua mfukoni alikutwa na tiketi ya basi la Ratco express iliyokuwa na jina la ely family mdundo kutoka Tanga kwenda dsm iliyokatwa Novemba  04 mwaka huu ambayo ilitakiwa kutumika  Nov 6 mwaka huu

Kwa mujibu wa taarifa kutoka jeshi la Polisi Mkoani humo Inadhaniwa kuwa marehemu alikuwa ni mhamiaji haramu.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya serikali wilaya ya mbozi. Uchunguzi zaidi wa tukio hili unaendelea.

Hata hivyo katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya  linawashikilia raia wanne wa nchini kongo kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

Wahamiaji hao ni pamoja na Hassan Kaula (18)  Katumba Asheri (20) Issah lukimbana (20) na  Ibele Buma (20).

Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 10.12.2014 majira ya saa 13:20 mchana katika msako uliofanyika huko katika eneo la kasumulu mpakani, Kata ya Ngana Wilaya ya Kyela,  Mkoa wa mbeya huku   Taratibu za kuwakabidhi idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea.


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top