Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 Waziri wa Maliasili na Utalii Razalo Nyarandu,

Na Mwandishi wetu,Mbeya
SERIKALI Nchini, imeamua kuachana na maeneo ya ardhi ya wananchi wa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya, ambayo yalipendekezwa kuingizwa kwenye hifadhi ya Taifa ya Tanapa.

Maeneo hayo ya wananchi yenye ukubwa wa kilomita za mraba 10,000 yamedaiwa kuidhinishwa na kamati ya ushauri ya mkoa wa Mbeya (RCC) kwa ajili ya kuingizwa kwenye hifadhi ya Tanapa jambo lililosababisha kuibuka kwa migogoro baina wananchi na Tanapa.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mbeya jana, Waziri wa Maliasili na Utalii Razalo Nyarandu, alisema serikali imeamua kuachana na maeneo hayo ya wananchi ambayo yalipendekezwa na uongozi wa Mkoa wa Mbeya kuingizwa kwenye hifadhi ya Tanapa.

Alisema, moja ya taratibu ambazo Mkoa unapaswa kuzifuata ni pamoja na kutenga fedha za fidia za kuwalipa wahanga hao pamoja na kuwaandalia maeneo husika ambayo miundombinu yake itakuwa imekamilika.

Naye Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Modestus Kirufi, alitumia nafasi hiyo kuishukuru serikali kwani uamuzi huo umesaidia kupunguza idadi ya migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikishamiri katika eneo hilo la Wilaya ya Mbarali.
mwisho.


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top