| Mkuu wa Mkoa wa mbeya Abbas Kandoro (katikati) akiwa pamoja na viongozi na wakuu wa wilaya ya mkoani humo katika mkutano na waandishi wa habari juu ya ukamilishwa wa zoezi la ujenzi wa maabara. |
SERIKALI ya Mkoa wa Mbeya, imeweza kutekeleza agizo la
Rais Jakaya Kikwete la ujenzi wa maabara kwa asilimia
95.45 kwa shule 696 zilizopo mkoani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo jijini Mbeya , Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbasi
Kandoro, amesema Mkoa wa Mbeya unajumla ya shule za sekondari 696
zinazomilikiwa na serikali na kati ya hizo shule 602 zimekamilisha ujenzi wa
vyumba hivyo vya maabara.
Kandoro amezitaja
halmashauri ambazo tayari zimekamilisha zoezi hilo kuwa ni Halmashauri ya
Mbeya, ambayo inajumla ya shule 27 za sekondari na maabara zilizokuwa
zikihitajika ni 81 na zote zimekamilika
sambamba na vitendea kazi vyake.
Amesema, halmashauri nyingine ni Kyela ambayo inajumla ya
sekondari 22 uhitaji wa maabara ulikuwa ni 66 na zote zimekamilika ikifuatiwa
na halmashauri ya Mbozi ambayo inajumla ya sekondari 40 maabara zilizokamilika
ni 117 kati ya 120 zinazohitajika.
Amesema, ujenzi wa vyumba hivyo vya maabara umeenda
sambamba na tarehe ya mwisho aliyoitoa Rais ya kwamba ifikapo mwezi Desember
mwaka huu, halmashauri zote nchini ziwe zimekamilisha ujenzi huo wa maabara.
Amesema, vyumba vya maabara 94 sawa na asilimia 4.55 ujenzi wake bado
unaendelea lakini ifikapo mwezi Desember
mwaka huu vitakuwa vimekamilika kwani matengenezo yaliyobakia ni madogo madogo.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa amesema halmashauri ya Mbarali ambayo imekamilisha ujenzi huo wa maabara 48 kati ya
48 zilizokokuwa zikihitajika huku
halmashauri ya Busokelo ambayo
inajumla ya shule 15 maabara zilizokamilika ni 41 kati ya 45 zinazohitajika ,
halmashauri ya Chunya shule zilizopo 20 maabara
60 zilizokamilika ni 18.
Hata hivyo, Kandoro amesema kuwa halmashauri ya Ileje
inajumla ya shule 19 na maabara zilizokamilika 51 kati ya 56 zinazohitajika
huku Jiji la Mbeya likiwa na shule 31
maabara zinazohitajika ni 93 kati ya hizo maabara 89 zimekamilika.
Mwisho.






Post a Comment