| Mkuu wa wa mkoa wa mbeya Abbas Kandoro akimkabidhi jezi Mwenyekiti wa Madhehebu ya Dini Mkoa wa Mbeya, Askofu wa kanisa la Anglikana Mkoa wa Mbeya, John Mwela |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Desember 9, mwaka huu
katika kuadhimisha miaka 53 ya uhuru viongozi wa dini wanatarajia kujitupa katika
Uwanja wa Sokoine wa Jiji la Mbeya na kulisakata kabumbu kwa lengo la kudumisha
amani iliyopo nchini.
Mtanange huo utawajumisha Masheikh,Maimamu,Maaskofu,Wach ungaji, Mapadre na
viongozi wote wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya, huku mgeni rasmi atakuwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Abbasi Kandoro.
Akizungumza jijini Mbeya
leo, Desember 6,2014, Mwenyekiti wa Madhehebu ya Dini Mkoa wa Mbeya, Askofu wa
kanisa la Anglikana Mkoa wa Mbeya, John Mwela, alisema mwamuzi wa mpambano
huomgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro.
Amefafanua kuwa viongozi
hao wa dini tayari wameshaanza mazoezi kwa jili ya kujiweka tayari kwa ajili ya
kufanya vizuri katika mtangane huo wa kuhamasisha amani na ulivu nchini.
Amesema, mpaka sasa kamati ya maandalizi imepokea timu moja ya Kamati ya ulinzi
na Usalama ya Mkoa wa Mbeya kushiriki mtanange huo na kwamba bado kamati imetoa
nafasi kwa timu mbalimbali za kijamii kufika kujiandikisha.
Amebainisha kuwa , michezo itakayochezwa
siku hiyo ni mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta kamba, kukimbiza kuku pamoja
kukimbia kwenye magunia hivyo amewataka wananchi kujitokeza siku hiyo
kushuhudia mtanange huo .
Hata hivyo, viongozi wa
madhehebu ya dini, wameonyesha kutotishwa na wapinzania hao kwani wao wamedai
kuwa timu yao ipo kamili na kwamba siku hiyo inatarajia kuibuka na ushindi.
Mwish







Post a Comment