Na Boniface Wambura,Dar es salaam
Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kinarejea leo Dar es Salaam
kutoka Bulyanhulu mkoani Shinyanga ambapo kiliweka kambi kwa ajili ya mechi ya
kimataifa dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu.
Timu hiyo ambayo leo asubuhi imefanya
mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, itatua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya Fastjet saa 12.30 jioni na
kwenda moja kwa moja kambini hoteli ya Tansoma.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager kesho (Desemba 7 mwaka huu) itafanya mazoezi asubuhi na jioni
kwenye viwanja vya Gymkhana wakati keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) itafanya
mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Taifa.
Nayo timu ya Taifa ya Burundi inatua
nchini keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya Kenya
Airways. Kikosi hicho kitafikia hoteli ya Tiffany Diamond kitakwenda moja kwa
moja Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kitafanya mazoezi kuanzia saa 11
jioni.
Kiingilio cha mechi kati ya Tanzania na
Burundi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni
kitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya raungi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B
na C ni sh. 5,000 tu.






Post a Comment