Mwanablogu maarufu lakini anayezusha mzozo Kenya ameshtakiwa kwa kumdharau rais, kufuatia ujumbe alioandika kwenye mtandao wa kijamii twitter mapema wiki hii.
Robert Alai anashutumiwa kwa kumuita Uhuru Kenyatta rais ambaye haja komaa kupitia ukurasa wake wa twitter.
Amekana mashtaka na akaachiliwa kwa dhamana ya dola elfu mbili.
Robert Alai amekumbwa na mzozo mara kadhaa kutokana na anayoyaandika kwenye ukurasa wake wa twitter.
Miaka miwili iliyopita alikamatwa na kuhojiwa kwa kutuhumu kwamba msemaji wa serikali anapanga kumuua.
Leo amefikishwa mahakamani kukabiliwa na mashtaka ya kunuia kumtusi rais.
Waendesha mashtaka wameiambia mahakama kwamba huenda wakaongeza mashtaka dhidi yake punde uchunguzi utakapokamilika.
Wakili wake ambaye ni seneta maarufu Kenya, amepinga jaribio la serikali kumnyima dhamana.
Hakimu anayesikiliza kesi amemuamuru kutoandika ujumbe kama huo katika mitandao yote ya kijamii wakati uchunguzi na kesi dhidi yake inpoendelea.
Alai ana wafuasi zaidi ya laki moja kwenye ukurasa wake wa twitter, na anatambulika kwa kuwa mkosoaji mkali wa serikali.CHANZO BBC
Post a Comment