Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Muonekano wa Ziwa Ngozi  lililopo   katika eneo la Mbeya One Wilayani Rungwe Mkoani  Mbeya. 
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Serikali imeendelea na jitihada zake mbalimbali za kuhakikisha wananchi wake hususani waishio vijijini wanaendelea kupata huduma ya umeme .

 Hatua hiyo inakuja kufuatia shirika la umeme nchini Tanzania (TANESCO)kuanzisha wa mradi wa uzalishaji umeme  kutumia ‘Joto ardhi’ lililopo katika Ziwa ngozi lililopo Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya .

 Kauli hiyo imetolewa jij Mbeya na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) Felchesmi Mramba, wakati wa mkutano mkuu wa Baraza la wafanyakazi  wa shirika hilo.

Amesema, mradi huo unaendeshwa na Kampuni ya Gothemo ambayo tayari ipo Mkoani Mbeya ikiendelea na kazi za awali za kuweka miundombinu pamoja na uboreshaji wa maeneo kabla ya kuanza kufua umeme huo kwa kutumia  joto ardhi.

Alisema, kupatikana kwa umeme huo kutasaidia kupunguza tatizo la umeme  pamoja na kushusha gharama ya huduma kwa watumiaji wa majumbani na viwandani hususani wakazi wa Mkoa wa Mbeya.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) Felchesmi Mramba


 Amesema tafiti mbalimbali zimefanyika na kubaini uwepo wa nishati ya umeme kwenye Ziwa hilo pamoja na kwenye Bonde la Mto Songwe kutokana na  kuzungukwa na miamba ya mawe ambayo hutoa joto linaloweza kuzalisha nishati hii ya umeme.

Ziwa hilo lipo katika eneo la Mbeya One Wilayani Rungwe Mkoani  Mbeya likiwa na urefu wa mita 150 kutoka kilele cha milima inayozunguka ziwa , ambapo kutoka usawa wa maji kina cha maji ni urefu wa mita 73 na ukubwa wa eneo lenye maji ni kilomita sita hadi 10 za mraba na lina ukubwa wa kilometa za mraba 3.75.

Wataalam wanaeleza kuwa ziwa hilo limetokana na volcano , limezungukwa na misitu mizuri ya asili ya kitropiki hali nzuri ya hewa na tulivu.

Ili kulifikia ziwa hilo unalazimika kutembea kwa mwendo wa kati ya dakika 45 na saa 1 kutoka kijijini Mbeye One ambacho kipo barabara kuu ya Mbeya-Kyela.

Pia kutoka katika kilele cha milima inayozunguka ziwa hilo unalazimika kushuka kwa zaidi ya dakika 45 huku ukilazimika kushuka kwa kutumia mizizi migumu ya miti ya asili iliyopo katika msitu mnene kwasababu ya mteremko mkali kuelekea katika ziwa hilo.
Mwsisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top