Na Boniface wambura,Dar es salaam
Timu ya Taifa ya
Rwanda (Amavubi) inawasili Mwanza, Januari 21 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya
kirafiki ya kimataifa dhidi ya Taifa Stars Maboresho itakayochezwa kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
Amavubi
yenye msafara wa watu 26, wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi itawasili
kwa ndege ya RwandAir na siku hiyo hiyo jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa
CCM Kirumba. Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya JB Belmont.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaingia kambini keshokutwa
(Januari 18 mwaka huu), na siku inayofuata itakwenda Mwanza tayari kwa ajili ya
mechi hiyo itakayofanyika Januari 22 mwaka huu.
Kikosi
hicho cha Kocha Mart Nooij ambacho ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo
za michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN) kinaundwa
na wachezaji 26.
Mwisho
Post a Comment