Meneja wa Benki ya Posta Mkoa wa Mbeya Humphery Julius Akikabidhi fedha hizo kwa mmoja washindi , Rehema Moses |
Na
Mwandishi wetu, Mbeya.
BENKI
ya Posta Mkoa wa Mbeya, leo imewakabidhi zawadi ya dola 300 za Marekani
washindi watatu wa promosheni ya Shindano la utumiaji wa huduma ya
kibenki kupitia akaunti ya Western Union.
Akikabidhi
fedha hizo kwa washindi hao, Meneja wa Benki ya Posta Mkoa wa Mbeya, Humphery
Julius, alisema washindi hao watatu ambao ni Alex Robart, Rehema Moses na
Godfrey Mwakajila wamepatikana baada ya droo iliyochezeshwa Jijini Dar es
Salaam .
“Washindi
hawa ni miongoni mwa washindi 13 ambao walishinda promosheni hii iliyokuwa
inashindaniwa kwenye Matawi yote ya Benki ya Posta yaliyopo nchini
Tanzania,”alisema.
washindi watatu wa promosheni ya Shindano la utumiaji wa huduma ya kibenki kupitia akaunti ya Weastern Union. |
Alisema,
shindano hilo lilijikita zaidi kwa watumiaji wa benki hiyo kupitia akaunti ya
Weastern Union lakini kwa wale waliokuwa wakipokea tu.
venac2002yahoo.co.uk
Aidha, Meneja huyo alitoa
wito kwa wakazi wa Mbeya, kujiunga na huduma za Benki hiyo kwani zimeboreshwa
na kuwafanya wateja wake kwenda na wakati katika shughuli zao zakujiletea maendeleo.
Hata
hivyo, akizungumzia zawadi hiyo, Mshindi Godfrey Mwakajila mkazi wa Uyole
Jijini Mbeya, alisema kiasi hicho cha fedha amekipata kwa muda muafaka kwani
kitasaidia kumaliza tatizo la ada ya shule ya mtoto.
Mwisho.
Post a Comment