Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
NA MWANDISHI WETU,TANGA.

TIMU ya Coastal Union imeondoka mkoani Tanga leo imeondoka alfajiri
kuelekea Mkoani Shinyanga ikiwa na wachezaji 20, walimu wawili na
viongozi wa timu hiyo tayari kwa kucheza mechi yao ya Ligi kuu
Tanzania bara dhidi ya Stand United itakayopigwa kwenye uwanja wa
Kambarage mjini humo.

Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa wiki endi hii ikiwa ni muendelezo wa
michuano ya Ligi kuu soka Tanzania Bara ambapo timu hiyo itaingia
uwanjani hapo ikiwa na matumaini ya kuweza kufanya vema baada ya
kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza

Msafara wa timu hiyo unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Coastal Union, Albert Peter ambaye amesema kuwa mara baada ya
kuwasilia mkoani humo watafanya mazoezi madogo madogo kabla ya mechi
hiyo inayotarajiwa kuchezwa Jumamosi wiki hii.

Akizungumzia hali za wachezaji wa timu hiyo, Kocha Mkuu, Mkenya James
Nandwa amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuhakikisha wanafanya
vizuri kwenye mechi hiyo ili kuweza kusogea kwenye nafasi za juu
kwenye msimamo wa Ligi kuu.

Amesema kuwa licha ya michuano hiyo kuwa na upinzani mkubwa lakini wao
wamejithatiti vilivyo ili kuweza kucheza kwa umakini ambao
utawawezesha kupata matokeo mazuri.

Hata hivyo amewataka wapenzi na mashabiki wa soka mkoani Tanga
wanaoishi mkoani Shinyanga kujitokeza kwa wingi kwenye mechi hiyo
lengo likiwa kuwapa hasama wachezaji wa timu hiyo.

Timu ya Coastal Union itaingia kwenye mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu
ya kupata sare kutokufungana nyumbani dhidi ya Polisi Morogoro ambapo
hivi sasa ina pointi 13 ikiwa nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi
kuu.

Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top