Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This



Kufuatia kuhusishwa na sakata la uchotwaji wa
mabilioni ya fedha katika akaunti ya Tegeta
Escrow, Waziri wa Nishati na madini Profesa
Sospeter Muhongo ameamua kumuandikia barua
Raisi ya kujiuzulu wadhifa wake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini
Dar es Salaam, Profesa Muhongo ameelezea
furaha yake ya kupatikana kwa maendeleo ya
haraka katika wizara yake kwa kipindi chake
akisema kuwa nidhamu na uwajibikaji vilikuwa
dira ya maendeleo wizarani hapo.
Profesa Muhongo amekwenda mbali zaidi na
kueleza kuwa anaamini kujiuzuru kwake
kutaisaidia Serikali na Bunge kutuliza malumbano
ya Sakata hilo ambalo linazidi kurudisha nyuma
maendeleo ya nchi.
Amesema yeye si mwizi na hawezi kuuza utu
wake kwa kupewa rushwa ili kuwakandamiza
watanzania.
“Nimeamua kujiuzuru kwa dhati kabisa bila
kushinikizwa na mtu yeyeote, inaonekana mimi
ndiyo nitamaliza mjadala huu wa sakata la
Escrow, tuna mambo mengi ya kitaifa
yanayotakiwa kujadiliwa lakini watu wamekazana
na Escrow, nimemuandikia Rais barua rasmi ya
kujiuzuru wadhifa wangu, amesema Profesa
Muhongo.
Amesema pamoja na kujiuzuru anatarajia
mapema kuzungumza na watanzania ili
kuwaeleza ukweli wa sakata la Escrow na
kujiuzuru kwake ili kuvunja majungu
yanayoendelea kuitesa Tanzania na watu wake.
Amesema yeye amelelewa katika malezi yenye
maadili mema na kwamba tokea alipomaliza
masomo yake aliaswa kutopokea ama kutotoa
rushwa hivyo hawezi akapokea rushwa kwa ajili
ya kuutukana utu wa mtanzania hicho ndicho.kinachomgharimu.
mwananchi. chanzo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top