Na Emanuel Madafa,mbeya
KUTOKANA na mkondo wa hali ya hewa uliombata maji maji
unaotoka nchini Congo, kuvamia anga la Mkoa wa Mbeya na kusababisha hali mbaya
ya hewa , leo ndege ya Fastjet
imeshindwa kutua na kulazimika kurejea Jijini Dar es Salaam.
Mkondo huo wa hewa , umetajwa kuvamia eneo la uwanja huo dakika
30 kabla ya ndege kutua katika uwanja wa Songwe, hali iliyosababisha
rubani wa ndege kuuzunguka uwanja huo zaidi ya mara mbili na mwishowe kurejea
tena Jijini Dar es Saalam.
Akizungumzia tatizo hilo, Meneja Mamlaka ya hali ya hewa Nyanda za
Juu Kusini, Issa Mohamed, alisema saa moja kabla ya ndege hiyo kutua hali ya
hewa ilikuwa vizuri, tatizo limejitokeza ndani ya nusu saa baada ya mkondo huo
wa hewa uliombatana na maji maji unaotokea
nchini Congo kuvamia eneo la uwanja wa ndege wa Songwe na
kusababisha hali ya hewa kuchafuka.
Amesema, Mkoa wa Mbeya upo karibu na misitu ya Congo hivyo baada
ya hali hiyo kuvamia asubuhi ilikutana
na mambonde na tabaka la chini likiwa na ubaridi kuliko hali yenyewe ya kawaida ndani ya nusu
saa kabla ya ndege hiyo kutua.
Aidha, amesema tatizo hilo haliwezi kutatuliwa kwani ni mabadiliko
ya hali ya hewa, jambo linalotakiwa kufanywa na mamlaka ya ndege ni (TIAA)
inaweka taa za muda ambazo humwezesha
rubani kutambua njia sahii wakati anatua hata kama hali ya hewa itakuwa mbaya.
Naye, Mratibu wa shughuli za ndege kutoka Kampuni ya Fastjet Mkoa
wa Mbeya, Omary Idrisa, amesema ndege hiyo imeshindwa kutua kutokana na hali ya
hewa kuwa mbaya hivyo kulazimika kugeuza Jijini Dar es Salaam ikiwa na zaidi ya
abiria 100.
Amesema kwamba ndege hiyo ilitakiwa kutua saa mbili asubuhi na dakika 25
na kuruka saa tatu na dakika tano, ikatua leo majira ya saa tisa mchana na kuondoka
saa 11 za jioni kwa mujibu wa taarifa kutoka mamlaka ya hali ya hewa.
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songwe, Valentine Kadeha, alikiri
ndege hiyo kushindwa kutua kwenye uwanja huo, hivyo kulazimika kugeuza
Jijini Dar es Salaam kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.
Hii ni mara ya pili ya ndege ya Fastjet kushindwa kutua katika
kipindi cha wiki tatu ndani ya mwezi huu wa January 2015.
MWISHO
Post a Comment