Kijana huyo ambaye ni teja akisimulia kilicho mkuta mara baada ya kukwapua simu ya mama huyo ambapo aligandishwa kwa zaidi ya masaa 7. |
Fimbo aliyoshika ndiyo iliyomsaidia kumpa nguvu ya kutembea ambayo nayo ilitoewa na mama huyo kama sehemu ya kinga na ngao anayotumia mganga huyo katika shughuli zake za kitaabibu |
Kijana Ommary baada ya kuachiwa huru na mganga huyo |
Mganga huyo mwenye koti akitoa masharti kwa mtuhumiwa wake . |
Picha na David Nyembe wa Fahari News |
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja aliyefahamika kwa
jina Ommary Said (20) Mkazi wa Sokomatola jijini mbeya amejikuta katika wakati
mgumu mara baada ya kudaiwa kukwapua simu ya mmoja wa abiria katika kituo hicho
cha mabasi jijini hapa na kugandishwa kwa zaidi ya masa7.
Tukio hilo la aina yake limetokea leo jijini hapa ambapo
inadaiwa kuwa kijana huyo katika harakati zake za kutafuta abiria aliingia
anga mbaya ambapo alikwapua simu ya
mmoja wa abiria na kutokomea nayo ambapo muda mchache mara baada ya kukwapua
simu hiyo alipiga hatua chache kisha kuganda hali ambayo iliibua mshangao kwa
watu waliopo katika eneo hilo la stendi kuu ya mabasi jijini hapa.
Inadaiwa kuwa kijana huyo Omary Saidi (20) mkazi wa Sokomatola ambaye
pia ni mtumiaji wa dawa za kulevya(Teja) mara baada ya kuchukua simu hiyo alihisi hali
tofauti ambapo alirudi na kumkabidhi mtu huyo alijitambulisha kwa jina Chiku Ramadhani kutoka Tabora ambaye anadaiwa
kuwa ni mganga wa kienyeji huku akitoa sauti ya huruma kwakuomba asamehewe
kwa kitendo hicho.
Akizungumzia tukio Mganga
huyo Chiku Ramadhani, amesema aliwasili Jijini Mbeya jana January 21 akitokea
Jijini Dar es Salaam, akiwa katika eneo la stendi kuu, aliingia kwenye moja ya
mgahawa kwa ajili ya kupata chakula, alipomaliza alienda kunawa mikono huku
simu yake akiwa ameicha kwenye meza aliyokuwa akiitumia.
Alisema, aliporejea alishangaa kumuona kijana huyo akiwa amesimama
kwenye eneo la karibu na meza hiyo huku kwenye mikono yake akiwa ameshika simu
yake na kumtaka aondoke jambo ambalo lilikuwa gumu kwa kijana huyo kutokana na
kushindwa kunyanyua miguu yake.
“Mimi nimeingia hapa stendi juzi nikitokea Dar, hivyo niliingia
kwenye mgahawa huu kwa ajili ya kupata chakula, nilipomaliza nilienda kunawa
mikono huku simu yangu nikiwa nimeicha kwenye meza lakini niliporejea
sikuiona simu pale nilipoicha zaidi nilishangaa kumuona kijana huyu akiwa
amesimama huku simu ikiwa mikononi mwake,”alisema.
Akizungumzia hilo, Kijana Omary Ramadhani, alikiri kuchukua simu
ya dada huyo ambayo alikuwa ameishika mkononi huku akiendelea kuomba
msamaha na mganga huyo kusikiliza kilio cha teja huyo na kumuachia huru.
“Nimefanya kazi ya upiga debe kuanzia jana jioni hadi usiku
sijapata kitu, hivyo nilivyoiona simu hii niliamua kuichukua na lengo likiwa
nikaiuze kwani sijapata chakula(Unga), hali yangu ni mbaya naombeni
mnisamehe,”alisema teja huyo.
Aidha, baada ya tukio hilo kumalizika, mganga huyo alionekana
kuvutiwa na watu ambao walionyesha nia ya kusaidiwa matatizo yao ambapo alianza
kuendesha shughuli zake za kuagua zilizoambatana na upigaji wa ramli kitendo
ambacho kimepigwa marufuku na serikali.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Norman Sigalla, akizungumzia
tukio hilo, alisema, serikali imewapiga marufuku waganga wote nchini kuendesha shughuli
hizo zikiwa zimeambatana na upigaji wa ramli hivyo mganga huyo anakiuka sheria
na taratibu za nchi.
Hata hivyo, alisema waganga hao wanatakiwa kufuata taratibu na
maelekezo kutoka Baraza la Tiba za asili Nchini, ambazo zimekuwa zikiweka
bayana masuala yanayopaswa kutekelezwa na kufanywa na waganga hao au matabibu
wa tiba asili.
Mwisho
Post a Comment