Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Kikao kilichopangwa kifanyike leo, kimehairishwa ghafla, huku tayari wadau na wsanii wakiwa tayari wapo ukumbini. Kikao hicho kilikuwa kifanyike chini ya wizara tatu ambazo ni Wizara ya Vijana Utamaduni na Michezo,Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya fedha kuhusuana na bei za filamu za hapa nchini.
Akielezea kile  kilichojiri, mwigizaji Salma Jabu “Nisha”amabe alikuwa ni moja kati ya walio hudhuria kikao hicho, alisema
“Kikao hakikufanyika, kimehairishwa.umeona wapi mtu utengeneze filamu halafu inapopangwa bei usiwepo?kisa eti tunasimamia kushusha bei na wao wasiwalalie wananchi dah yaani... kuna watu wanafanya vitu kwa maslahi ya familia zao wakisahau hayo maslahi yanatoka kwa wananchi.. hivi kuuza elfu 3 ukapata faida ya na kuuza elf 1500 ukapata faida ya  na kuuza elf 1500 ukapata faida ya na kuuza elf 1500 ukapata faida ya 20% na kuuza elf 1500 ukapata faida ya 80% 
Akizungumzi msimamo wake, Nisha alifunguka;
"Kwa msimamo wangu kama mfanya biashara wa filamu na msanii Tanzania,napendekeza bei ishuke ili watu wote wawe na uwezo wa kununua,haiwezekani tuwauzie mashabiki filamu kwa elf 3 wakati elf 1500 pia tunapaa faida,kwanini mununue filamu kwa bei kubwa filamu iliyokatwa katwa ambayo unaweza ifanya iwe part 1? Huo ni wizi wa wazi wazi
Steps entertainment imeleta vifaa vya kuzalisha kazi hapa nchini faida inapatikana kwanini tuuze bei kubwa?ili kunufaisha pirates wanaouza 500 kwa kazi za kuiba,kila siku tunapigana na pirates (wizi wa kazi za wasanii)lkn bado wapo,leo kushusha bei kwa nia ya kuzuia kuibiwa msanii na mnunuzi kuna wanaopinga,Natamani bei ishuke ili hawa wanaokodisha waanze kuuza wapate faida na wao,na wanao zikodi waanze kununua.
Ni aibu kubwa kwa tasnia kama hii kuuza nakala elfu 20 tu wakati watanzania tupo zaidi ya ml.47,sio kwamba haiuziki inauzika sana ila wanaofaidika ni wale wanaoiba".

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top