Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro akionyesha hati kuashiria kuzinduliwa kwa mpango huo kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Mariam Mtunguja kushoto  ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Profesa Norman Sigalla..

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza na wananchi waliohudhuria sherehe hiyo ya uzinduzi katika kiwanja cha michezo kijiji cha Iziwa kata ya Nsoho jijini Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akishiriki zoezi la upandaji miti


Mshereheshaji wa sherehe hiyo Mc wa Kimataifa Ndugu Charles Mwakipesile



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akikabididhi mizinga ya nyuki kwa Diwani wa kata hiyo


Afisa maliasiri na utalii Joseph Butuyuyu akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango huo.

Kikundi cha maigizo kutoka kihumbe kikitoa burudani katika sherehe hiyo.




Na Emanuel Madafa,Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro, amewataka wananchi kutoweka mbele maslahi ya fedha katika shughuli za utunzaji wa mazingira hususani kwenye vyanzo vya maji na badala yake watambue umuhimu na wajibu  wa kulinda  na kutunza mazingira.


Kandoro, ametoa kauli hiyo leo, wakati  wa uzinduzi wa mpango wa  kuhifadhi mazingira kwenye safu ya milima ya Mbeya eneo la Nsoho Kata ya Iziwa iliyomo ndani ya Jiji la Mbeya.

Amesema, suala lawatu  kutegemea fedha kwenye  utunzaji wa mazingira,  umepitwa na wakati badala yake amewataka kutambua kuwa fedha hizo ni sehemu ya kuongeza   chachu ya kusaidia kusukuma suala hilo.


Aidha, amewataka wananchi hao wakaachana na  tabia ya kukata miti ovyo kwa ajili ya uchomaji wa nishati ya mkaa kwani mapaka sasa jumla ya  vyanzo 40 vya maji vimekauka katika Mkoa wa Mbeya kutokana na uharibifu wa mazingira.


Hata hivyo,  amesema ili kufanikisha mpango huo nivema  kila mmoja  akatambua wajibu wake katika suala la utunzaji wa mazingira pamoja kuachana na tabia ya kutaka fidia mara serikali inapo taka kupanda miti katika eneo husika ili kukabiliana na hali hiyo.


 Katika tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro, amekabidhi  mizinga ya nyuki  kumi kwa uongozi wa kijiji hicho cha Nsoho.



Kwa upande wake afisa misitu na maliasili mkoa wa mbeya ndugu Joseph Butuyuyu amesema katika kutekeleza mpango jumala shilingi mili28.8 baadhi ya wadau mbalimbali wametoa fedha hizo ili kufanikisha azma hiyo.

Mwisho.

 JAMIIMOJABLOG

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top