Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya Ndugu Veronica Kessy |
Na Emanuel
Madafa,Mbeya
MAHAKAMA
Kuu (MBEYA), inatarajia kuwafungulia kesi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rungwe
Veronica Kessy na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mek One Mohamed Awadh , baada ya
kukiuka agizo la mahakama lililowataka kutofanya jambo lolote katika
kituo cha mafuta cha Gapco mpaka kesi ya msingi namba 6/2013 iliyopo kwenye
mahakama ya Wilaya itakapotolewa maamuzi.
Agizo hilo
lilitolewa na Mahakama kuu Oktoba 8, 2013 na Jaji Atuganile Ngwala, baada
ya Halmashauri ya Rungwe ambayo inamiliki kituo hicho cha mafuta kudaiwa
kuingia mkataba na Kampuni ya mafuta ya Mek One , wakati mkataba wa awali
walioufanya na kampuni ya mafuta ya GAPCO haujamalizika muda wake, kinyume cha
sheria namba 114(i) (k) sura ya 16 ya mwaka 2002.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Msajili wa Mahakama, Aron Lyamuya,
alisema kutokana na wahusika hao kukiuka agizo hilo lililotolewa na Jaji
Ngwala, Mahakama hiyo inatarajia kuwafungulia kesi watuhumiwa hao.
Amesema,
Mahakama hiyo ilipokea maombi kutoka kwa Kampuni ya mafuta ya
GAPCO yenye namba 76/2014 ambayo ilieleza kwamba mmiliki
huyo,halmashauri ya Rungwe kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa kampuni ya Mek
One, wameingia mkataba na kuanza kuendesha shughuli ya uuzaji wa mafuta
licha ya mahakama hiyo kuzuia.
Amesema,
kutokana na agizo hilo, mahakama inatarajia kuzungumza na Mwanasheria wa
serikali na ofisi ya upelelezi Mkoa wa Mbeya(RCO) ili kuona utaratibu wa
kuwafungulia mashitaka wawatuhumiwa wote wawili kutokana na kukaidi agizo hilo la Mahakama.
Mwisho.
Post a Comment